HAALAND NJIA NYEUPE KUTWAA BALLON D OR

 Hatimaye Erling Halaand ametwaa tuzo ya mchezaji bora  wa Ulaya mara baada ya kuwashinda Lionel Messi na Kelvin De Bruyne . Halaand anakuwa mchezaji wa kwanza kwa karne ya 21 kutoka nchini Norway na kushinda tuzo hiyo.


Msimu wa 2022/23 Halaand alijiunga na Manchester City akitokea Borussia Dortmund kwa dau la paundi milioni 50 na katika msimu huo alifanikiwa kufunga mabao 52 katika michezo 53 aliyocheza.Halaand likuwa mfungaji bora wa Premia Ligi baada ya kufunga mabao 36 katika mechi 38 na kuisaidia klabu yake kutwaa ubingwa wa ligi.

Halaand aliiwezesha Manchester City kutwaa ubingwa wa Ulaya kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo huku akifunga mabao 12 na kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo.

Mpaka sasa Halaand ameisaidia klabu yake kutwaa makombe ya Uefa Champions League,Uefa Super Cup,EPL na FA kama atafanikiwa kuisaidia klabu yake ya Manchester city kutwaa ubingwa wa klabu bingwa dunia basi ana asilimia 100 za kutwaa tuzo za ballon d or pamoja na fifa player of the year

Ikumbukwe halaand anamiaka 22 akiwa na jumla ya magoli 35 katika michezo 30 ya ligi ya mabingwa ulaya je ataweza kuvunja rekodi ya cristiano Ronaldo mwenye mabao 141 na Lionel Messi mwenye mabao 129.

Post a Comment

0 Comments