ERIK TEN HAG ATUMIE KOMBE LA DUNIA KUJITAFAKARI

 Manchester united inatushinda tabia kwa mambo inayoyafanya ndani ya uwanja na kutufanya tuamini tatizo si wachezaji bali kocha Erik Ten Hag. Haya yanaweza kusemwa kipindi hiki ambacho tumeshuhudia mabeki wa Manchester United wakifanya vizuri kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar.

Manchester United imesheheni mabeki bora tangu msimu wa 2021/22 na msimu ule ilifunga mabao 54 na kufungwa mabao 54 katika mechi 38 za EPL walizocheza sawa na uwiano( goal difference) 0. Combo ya Lindelof na Harry Maguire ilionekana kushindwa kuhimili washambuliaji wa timu pinzani na hata uwepo wa Varane ndani ya kikosi hicho haukuwa tija kutokana na majeraha yake ya mara kwa mara.

Msimu wa 2022/23 kocha Eric Ten Hag ameongeza idadi ya beki wa kati kutoka Ajax ambaye ni Lisandro Martinez. Sote tuliamini beki bora amepatikana na ni wakati sahihi kwa timu hiyo kuwa imara kama zamani. 

Mpaka naandika makala hii Manchester United imecheza mechi 14 za EPL na kufungwa mabao 20 kati ya 20 waliyofunga na kufanya wawe na goal difference 0.uwepo wa martinez, harry maguire, varane, Lindelof umeonekana hamna msaada kwa timu hiyo na hapo tunasema, je ni wachezaji wanaifelisha Manchester United au kocha Eric ten hag? 

Nimejaribu kukagua ubora wa mabeki wa Manchester United kupitia michuano ya kombe la Dunia ambapo wengi wamekuwa wakipata nafasi.

 HARRY MAGUIRE alikuwa nguzo muhimu sana kwa timu yake ya taifa Uingereza na mwalimu Southgate alikuwa akimtegemea kutokana na umahiri wake uwanjani, mpaka Uingereza inatolewa hatua ya robo fainali dhidi ya Ufaransa Harry Maguire alikuwa ni mchezaji tegemezi wa kikosi cha kwanza katika mechi 5 walizocheza. 

RAFAEL VARANE mpaka kufika fainali beki huyu amekuwa msaada mkubwa sana kwa ufaransa akicheza michezo 5 na timu yake ikifungwa mabao 4 katika mechi 6 walizocheza mpaka kufika fainali. Kocha Didier Deschamps amekuwa akimwamini nyakati zote tangu mwaka 2018 walipotwaa kombe la dunia na hata hata alipokuwa Real Madrid alikuwa bora mno swali ni je wapi Manchester United inafeli? 

LISANDRO MARTINEZ amejiunga na Manchester United msimu huu akiwa mchezaji pia mchezaji muhimu katika kikosi cha Argentina. Kocha Lionel amekuwa akimtumia Martinez kwa namna tofauti tofauti akicheza kama beki wa kati au kiungo mkabaji na amefanikiwa kuzimudu nafasi hizo sote katika michuano ya kombe la Dunia na sasa yupo fainali swali ni je Eric Ten Hag aliyemkuza pale Ajax ameshindwa kutengeneza combination bora zaidi? 

 kuna nyakati tunawalaumu viongozi kwa kufanya makosa mengi sana ya kiusajili, kuna nyakati tunawalaumu wachezaji kwa mwenendo wao mbovu lakini pia tunamlaumu kocha kama timu haitupi mategemeo yetu 

Huu ni wakati wa kumfuata Eric ten hag atuambie ni nini kimeikumba Manchester United kwa kushindwa kupata matokeo yenye tija. 

Kwa ukuta wa wachezaji hao kocha mwenye weledi anaweza kutumia mifumo mingi mno kama 3-5-2 kama unacheza mfumo huo na mbele yako una Casemiro, mc tomminay utashindwa kuwazuia wapinzani? 

Kwa wachezaji waliopo Manchester United na ubora walionao kocha wao ajitafakari kabla mambo hayajaharibika

Post a Comment

0 Comments