Nasser Al Khelaifi ndiye mwanadamu mwenye furaha zaidi nchini Qatar na dunia kwa ujumla katika fainali hizi za michuano ya kombe la Dunia 2022. Furaha ya Nasser inakuja baada ya vijana wake 11 akiwemo Messi, Achraf Hakimi na Mbappe wakiweka rekodi ya kufika nusu fainali na fainali.
Mwaka 2011 Nasser Al Khelaifi aliteuliwa Qatar Sports Investment kama raisi wa kampuni hiyo yenye mlengo wa kuwekeza katika michezo mbalimbali nje ya Qatar na mwezi October 2011 alichaguliwa kuwa raisi wa klabu ya PSG ya ufaransa ambayo anahudumu mpaka leo hii.
Mwaka 2011 Nasser Al khelaifi aliteuliwa kuwa mmoja ya wanakamati wa maandalizi ya kombe la dunia kwa mwaka 2022, michuano ambayo inaendelea mpaka sasa kwa michezo miwili iliyobaki kati ya Crotia dhidi ya Morroco kumtafuta mshindi wa tatu na fainali ya Argentina dhidi ya Ufaransa.
Akiwa ndani ya PSG aliweka mipango ya kuikuza thamani ya klabu hiyo ndani na nje ya ufaransa na alifanikisha hilo kwa kuwasajili wachezaji wenye majina makubwa akiwemo Zlatan Ibramovich, Edison Cavani, Neymar Jr, Kylian Mbappe, Messi na wengine wengi.
Sajili zilizofanywa na PSG chini ya raisi Nasser ziliongeza thamani kwa klabu hiyo na kufungua milango ya wadhamini na ufuatiliwaji wa klabu hiyo duniani kote.
Mbali na kufanikiwa masuala ya kiuchumi kwa PSG lakini pia Nasser amefanikiwa kwa kuwafanya nyota wake wawe gumzo kwenye michuano ya kombe la dunia Qatar ambako yeye anasimama kama mjumbe wa bodi ya maandalizi na usimamizi wa michuano hiyo kutoka Qatar na pia timu ya taifa ya Ufaransa imeingia fainali mahali ambapo yeye anafanya kazi kama raisi wa PSG na hata mchezaji bora na tegemezi anayekipiga Ufaransa ni kutoka klabuni mwake PSG
PSG imefanikiwa kupeleka wachezaji 11 na baadhi ya wachezaji hao walizifanikisha timu zao kufika Robo fainali, Nusu na fainali. Hayo ni mafanikio makubwa sana kwa raisi huyo na kunamjengea heshima ya kipekee kwenye ulimwengu wa soka. Hawa ni Baadhi ya nyota wanaomfanya Nasser Al Khelaifi awe na furaha zaidi kwa Mwaka 2022
ACHRAF HAKIMI
Nyota huyu wa Morocco mwenye miaka 24 alijiunga na PSG mwaka 2021 akitokea Inter Milan na amekuwa akitajwa kama modern right back(beki bora wa kisasa upande wa kulia). Mbali na kuvitumikia vilabu mbalimbali kama Real Madrid, Dortmund, inter milan na sasa Psg amekuwa ni nguzo imara kwa timu yake ya morocco na ameisaidia timu hiyo kufika nusu fainali huku wakifungwa mabao mawili pekee dhidi ya ufaransa katika michuano hiyo na sasa watacheza dhidi ya Crotia kumtafuta mshindi wa tatu.
KYLIAN MBAPPE
Mwaka 2018 Mbappe alishiriki michuano ya Kombe la Dunia nchini Russia na aliibuka na tuzo mbalimbali ikiwemo mchezaji chipukizi na mfungaji bora namba mbili wakati huo akiwa mgeni ndani ya PSG.
2022 Kylian Mbappe akiwa mfungaji bora wa Ligue 1 na mchezaji tegemezi kwa PSG anafanikiwa kuipeleka Ufaransa hatua ya fainali akiwa mchezaji tegemezi kwa kufunga mabao 5 pasi za mabao 2 katika mechi 5 alizocheza kwa wakati huu. Kama atafanikiwa kutwaa taji hilo kwa mara ya pili mfululizo basi tajiri Nasser Al Khelaifi atajiwekea rekodi zisizoshikika.
LIONEL MESSI
Nyota huyu mwenye tuzo 7 za Barron d or amezidi kuudhihirishia ulimwengu wa soka kama yeye ni mchezaji bora zaidi wa kizazi hiki baada ya kuisaidia timu yake ya Argentina kufika fainali ya kombe la dunia akifunga mabao 5 pasi za mabao 3 katika mechi 6 alizocheza.
Messi alisajiliwa na PSG mwaka 2021 chini ya Nasser Al Khelaifi kama mchezaji huru baada ya mikataba yake kumalizika ndani ya Barcelona.
Kwa wakati huu wa fainali itakayopigwa disemba 18 kila mmoja anajiuliza je tajiri Nasser Al Khelaifi atasimama upande wa Messi au Mbappe?
Binafsi namwona ndiye mtu pekee atakayekuwa na furaha siku ya fainali kwa sababu mmoja wa wachezaji wake atavaa medali ya ubingwa na inawezekana akaondoka na kiatu cha mfungaji bora na kuna uwezekano mchezaji bora wa michuano hii akawa Messi au Mbappe na hapo tunasema
"PESA INAWEZA KUNUNUA FURAHA"
0 Comments