BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA WAKO KAMILI GADO KUREJEA KILELENI MWA LIGI

 Kikosi cha maangamizi kinachonolewa na kocha Nabi limeonekana kuwa kamili gado kuelekea mchezo wa kesho jioni dhidi ya Azam FC. Yanga watakuwa uwanja wa nyumbani kuwakaribisha Azam kwenye mchezo huo muhimu wa NBC na wanakiu kubwa ya kupata ushindi baada ya kufanya vizuri kwenye michezo miwili ya ugenini.

Mchezo wa Kwanza Yanga walikaribishwa na Polisi Tanzania katika dimba la Sheikh Amri Abeid na mchezo kumalizika kwa Yanga kushinda mabao 2-1 huku mchezo wa pili Yanga akishinda mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union katika dimba hilohilo la Sheikh Amri Abeid wakijikusanyia pointi 6 na tofauti ya mabao 3. wapinzani wao wa jadi klabu ya Simba wanaongoza ligi kwa pointi 6 wakiwa na magoli 5 kwenye mechi mbili walizocheza.

Yanga wanapaswa kushinda mchezo huo ili waweze kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi wakijikusanyia pointi 9 kwa mechi tatu na kama watapoteza mchezo huo basi Azam atapanda mpaka nafasi ya 1 akiwa na pointi 7.

Mpaka sasa Yanga hakuna mchezaji mwenye majeraha na kuna uwezekano mwalimu Nabi akaanza na kikosi chenye wachezaji kama Djigui Diarra ,Shaban Djuma,Joyce Lomalisa,Dickson Job,Yannick Bangala,Khalid Aucho,Feisal Salum,Morrison,Aziz Ki,Moloko na Fiston Mayele .

Hawa hapa Yanga wakijiandaa na mchezo huo muhimu
Post a Comment

0 Comments