BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO TAREHE 06 /09/2022

 Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich imeingia katika mbio za kumuwania nyota wa Barcelona Gavi, huku Manchester United na Liverpool zikiaminika tayari zimeanza kumfuatilia kiungo huyo Mhispania mwenye miaka 18. (Bild, via Mail)

Napoli imekanusha kufanya mazungumzo na mshambuliaji mreno wa Manchester United Cristiano Ronaldo, 37, msimu huu. (Fabrizio Romano)

Ronaldo

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Ronaldo

Kocha wa Leicester boss Brendan Rodgers, 49, atajipatia kitita kinono kama atatimuliwa kufuatia klabu hiyo kuanza vibaya msimu wa ligi tangu ifanye hivyo mwaka 1983. (Mail)

Chelsea itanunua kiungo wa kati katika dirisha la mwezi Januari huku nyota wa kimataifa wa  Mexico Edson Alvarez, 24, akiwa ni kioaumbele chao cha kwanza. (Standard)

The Blues pia wako tayari kumpa mkataba mpya kiungo wake wa England Mason Mount, 23 baada ya mwenzake Reece James, 22, kusaini mkataba mpya wa miaka 6. (Telegraph)

Mount

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mount

Kocha mkuu wa AC Milan Stefan Pioli amefichua kwamba klabu hiyo inajiandaa kumpa mkataba mpya mshambuliaji wake mreno Rafael Leao, 23 huku kukiwa na ripoti za kuhususishwa na vilabu kadhaa ikiwemo Liverpool. (Liverpool Echo)

Mateo Kovacic anasema alimpendekeza beki Mcroatia wa RB Leipzig Josko Gvardiol, 20 kwenda Chelsea katika dirisha la usajili lililofungwa hivi karibuni. (Standard)

Mshambuliaji wa zamani wa Hispania Diego Costa, 33, anasafiri leo kwenda kukamilisha uhamisho wa wake wa kutua Wolves. (Telegraph - subscription required)

Costa

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Costa

Brighton wanajiandaa kufanya mazungumzo na Liverpool kwa ajili ya uhamisho wa mwezi Januari wa kiungo wa Ecuador n January Moises Caicedo, 20. (Tera Deportes, via Express)

Kiungo wa RB Leipzig raia wa Austria Konrad Laimer, 25, uhamisho wa dakika za mwisho kwenda Liverpool haukuwepo kufuatia tetesi kuzagaa masaa machache kabla ya dirisha kufungwa. (Standard)

Post a Comment

0 Comments