BETI NASI UTAJIRIKE

SIMBA WANAMPANGO GANI NA KIKOSI CHAO?

 Kikosi cha Simba kilichorejea jijini Dar es Salaam kutokea Sudan kwenye michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Asante Kotoko na Al Hilal kimeanza kuwapa mashaka mashabiki wake hasa kuelekea michuano ya kimataifa dhidi ya Nyasa Big Bullet.


Kikosi hicho kilicheza mchezo wa kirafiki asubuhi ya leo dhidi ya ARTA SOLAR 7 ya Djibouti na kuambulia kipigo cha bao 1-0 bao lilifungwa dakika ya 89 na mshambuliaji Manucho Athuman. Simba waliutawala mchezo huo na kufanikiwa kupiga mashuti mengi langoni mwa Arta Solar lakini hawakupata goli. 

Huu unakuwa mchezo wa pili kwa Simba kupoteza,Tarehe 31 walifungwa Bao 1-0 na Al Hilal mchezo wa kirafiki uliopigwa Sudan.

Tarehe 7 Septemba Simba itavaana na  KMC mchezo wa ligi kuu NBC na itasafiri kuelekea Malawi kucheza mchezo wa klabu bingwa Afrika kwa hatua ya kwanza dhidi ya Nyasa Big Bullets utakaopigwa tarehe 10 Septemba.

Tarehe 14 Septemba mchezo mwingine wa ligi kuu NBC utapigwa jijini mbeya dhidi ya Tanzania Prisons na tarehe 17 wataikaribisha Nyasa Big Bullets kucheza mchezo wa raundi ya pili dimba la Benjamin Mkapa.

Swali ni je kwa mwenendo huu mbovu wa michezo miwili dhidi ya Al Hilal na Arta Solar timu hii inaweza kusonga mbele kimataifa na kufanya vizuri michezo ya ligi kuu?

Post a Comment

0 Comments