BETI NASI UTAJIRIKE

SAIDO NTIBAZONKIZA KWISHA HABARI YAKE

 Nyota wa Geita, Mrundi Saido Ntibazonkiza ambaye amesaini mkataba na timu hiyo akitokea Yanga jina lake halijaonekana kwenye wachezaji wa timu hiyo wanaoiwakirisha kimataifa.Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa orodha ya wachezaji 40 ambao watashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika huku jina la Saido halimo katika orodha hiyo.

AMOspoti imefanikiwa kuzungumza na Katibu wa timu hiyo Simon Shija ili kuweza kufahamu hatua zinazoendelea.

"Mpaka sasa sijajua  nini kinaendelea kwa kuwa nilikuwa kwenye kikao kuanzia asubuhi .Lakini tulifuata utaratibu wote wa CAF hivyo sifahamu nini kimetokea, tunachosuburi ni barua rasmi itakayotupa maelekezo na hapo ndipo tutaweza kulizungumzia hili,"

Mchezaji huyo ambae ameonyesha uwezo wake kwenye mchezo wa kirafiki baada ya kutoa pasi za mabao katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Pamba.

 Haya hapa ni majina ya wachezaji wa Geita Gold






Post a Comment

0 Comments