BETI NASI UTAJIRIKE

MAPYA YAIBUKA KUHUSU KISINDA ,TFF CAF NA YANGA KUKAA MEZANI

  Sakata la usajili wa Tuisila Kisinda ndani ya Yanga limeanza baada ya klabu ya  kusisitiza kwamba imefanya kila kitu kwa wakati na mchezaji huyo ni mali yao lakini Shirikisho la Soka la Tanzania(TFF) limesema hapana.


Yanga wamekuwa katika vikao vizito na simu zisizokauka wakipambana kutumia wanasheria kukutana na Kamati ya Leseni pamoja na ile ya Sheria na Hadhi za wachezaji kusaka ufumbuzi wa usajili huo.

Wamesisitiza kwamba kwenye usajili walichomoa jina la majeruhi Lazarous Kambole na kumchomeka Kisinda kwa kumlipia faini Shirikisho la Soka la Afrika (CAF). Iko hivi; Kisinda ambaye yupo Yanga kwa mkopo akitokea Berkane ya Morocco iliyowauzia msimu uliopita baada ya kumalizika msimu wa 2020-2021. Yanga kupitia kwa Mkurugenzi wa Mashindano wa klabu hiyo, Saad Kawemba alisisitiza wameshakamilisha usajili huo kwa kulipa faini kutokana na kuchelewa kupeleka jina la mchezaji lakini wanashangaa kinachoendelea ndani ya TFF 

“Unajua wenyewe tunapata ukakasi kwenye ishu ya mchezaji huyo jina lake kushindwa kupitishwa wakati tayari tulishaomba kuondolewa kwa jina moja la mchezaji wa kigeni kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya muda mrefu,” alisema. 

“Tuliomba jina la Lazarous Kambole liondolewe ili kupisha jina la Kisinda kutokana na mchezaji huyo kuwa na majeruhi ya muda mrefu kwa makubaliano ya kuendelea kumtimizia kila kitu hadi dirisha dogo litakapofunguliwa.

“Tunashangazwa na taarifa ya TFF kwamba sisi tuna wachezaji 13 na tumekiuka kanuni sio kweli kwani tulikuwa na ombi maalumu kwa ajili ya kumtoa mchezaji mmoja na kumuingiza mwingine na tulifanya hilo kwa kuzingatia muda wa usajili.”

Kisinda yupo nchini na amekwishaanza mazoezi na wachezaji wenzake wa Yanga kama mambo yatakaa sawa basi mchezaji huyo atajiunga na Yanga.


Post a Comment

0 Comments