BETI NASI UTAJIRIKE

NINI KIFANYIKE KUINUSULU TAIFA STARS

 Taifa Stars imeendelea kuwanyima raha mashabiki wa soka nchini baada ya hii leo kupoteza mchezo wake wa pili dhidi ya Uganda the Cranes. mchezo huo muhimu wa kufuzu michuano ya CHAN 2023 raundi ya pili  uliopigwa nchini Uganda na Taifa Stars kufungwa mabao 3-0.


Mchezo wa raundi ya kwanza Taifa Stars ilifungwa bao 1-0 na kusababisha kocha mkuu wa wakati huo Kim Poulsen kuondoshwa katika afasi ya Kocha mkuu. Nafasi ya Kocha mkuu ilichukuliwa na Janza ambaye ni kocha mkuu wa Namungo akisaidiana na Mecky Mexime kama kocha msaidizi na Juma Kaseja akawa ni Kocha wa Makipa.

Matokeo hayo yanaifanya taifa Stars kukosa michuano ya CHAN 2023. Mbali na michezo hiyo Taifa Stars itakosa michuano ya kimataifa ikiwamo AFCON 2023 na  Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.


Kipigo hicho kimeonekana kuwakera mashabiki wa soka nchini na wameibua hoja ya nini kifanyike ili timu yetu ya taifa iwe bora? 


Post a Comment

0 Comments