BETI NASI UTAJIRIKE

NINI KIFANYIKE KUEPUSHA ANGUKO LA GEORGE MPOLE NA GEITA GOLD?

Msimu wa 2021/22 klabu ya Geita Gold ilifanikiwa kucheza ligi kuu NBC kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa. Geita Gold walionekana kuwa na mipango mikakati ya kufanya vizuri kwa msimu huo na walifanikisha kila kitu ikiwemo kumaliza nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi na mfungaji wao George Mpole kuwa mfungaji bora kwa kufunga mabao 17.


Msimu wa 2022/23 mambo yamebadilika ,George Mpole hana goli lolote lwa mechi 3 za ligi kuu alizocheza.Geita Gold wamevuna pointi 2 katika mechi 3 walizocheza. Mchezo wa kwanza walikutana na Simba na kuambulia kipigo cha mabao 3,mchezo wa pili walitoka suluhu ya bao 1-1 dhidi ya Azam na mchezo wa 3 wametoa suluhu ya mabao 1-1. Matokeo hayo yanaifanya Geita kushika nafasi ya 11. 

Tarehe 11 Geita Gold watakuwa ugenini kucheza mchezo wake wa kwanza kombe la shirikisho dhidi ya Hilal Alsahil ya nchini Sudan .Kwa mwenendo mbovu ilionao kwa mechi za ligi kuu siioni Geita Gold ikifanya mambo makubwa katika mechi hiyo.

Swali ni je nini kifanyike kuwanusulu kina mpole na anguko lao?

Post a Comment

0 Comments