BETI NASI UTAJIRIKE

MESSI NA RONALDO SIO HABARI TENA MBAPPE NA HALAAND WAINGIA TENA VITANI

 Vita mpya imeshaanza kwa msimu huu kati ya Kylian Mbappe anayekipiga PSG na Erling Halland anayekipiga Manchester City. kwa msimu wa 2021/22 Halaand na Mbappe waliweka rekodi nyingi kwa ligi zao za Ligue 1 Ufaransa na Bundesliga Ujerumani. 


Rekodi ndani ya ligue 1 na EPL

Mpaka sasa nyota hawa wawili wameshaweka rekodi mpya kwa ligi wanazocheza .Mbappe akiwa na PSG ndiye mchezaji anayeongoza kwa mabao 7 akicheza mechi 6 sawa na mchezaji mwenza Neymar JR.Mabao hayo yameisaidia PSG kufikisha pointi 16 katika mechi 6 walizocheza.

Halaand ameanza vyema kwa msimu huu akifunga mabao 10 katika mechi 6 alizocheza huku akifunga Hat Trick mbili mfululizo. Mabao hayo yameisaidia timu ya Manchester City kufikisha pointi 14.

Rekodi michuano ya UEFA 

Kwa msimu wa 2021/22 Kylian Mbappe akiwa na PSG aliweza kufunga mabao 6 kwenye michuno hiyo. Kwa msimu wa 2022/23 Mbappe ameshafunga mabao 2 dhidi ya Juventus . Matokeo hayo yanaifanya PSG kuongoza kundi H wakishinda mabao 2-1.Swali ni je Mbappe atamfunika Halaand kwa msimu huu?

Msimu wa 2021/22 Halaand akiwa na Borrusia Dortmund hakuwa na msimu mzuri. Kwa msimu wa 2022/23 Halaand amefanikiwa kufunga mabao 2 dhidi ya Sevilla .Matokeo hayo yanaifanya Manchester City kukaa kileleni mwa kundi G wakishinda mabao 4-0. swali ni Halaand atamfunika Mbappe.

Kwa msimu huu tusahau ile vita ya ronaldo na Messi na tuhamie kwenye hii vita nyingine itakayodumu kwa miaka 15 ijayo.

Post a Comment

0 Comments