BETI NASI UTAJIRIKE

TFF WAMUIBUA HAJI MANARA

 Chama cha mpira wa miguu Tanzania (TFF) kimeukataa usajili wa klabu ya Yanga kwa  mchezaji wake Tuisila Kisinda baada ya kushindwa kukidhi matakwa ya usajili.

Yanga walitangaza kumsajili mchezaji huyo kwa mkopo kutoka RS BERKANE lakini usajili huo umeonekana kuwa na utata. Hapo awali Yanga walipeleka majina 12 ya wachezaji wa kigeni likiwemo jina la Lazarous Kambole lakini baadaye walitaka jina hilo liweze kuondoshwa na kuweka jina la Tuisila Kisinda jambo lililokataliwa na TFF na kuzua mjadala kwa wadau wa soka akiwemo aliyewahi kuwa msemaji wa Yanga Haji Manara alinukuliwa akisema 

"Kumzuia Tuisila kisinda kucheza Yanga kwa sababu zisizokidhi masharti ya kanuni ni mwendelezo wa uonevu dhidi yetu. Kosa liko wapi wakati usajili wake umewahi kabla dirisha halijafungwa? Mwisho lini klabu kupangiwa muda wa kuwasilisha majina ya usajili? Iwe kwa wachezaji local au foreigners? 

"Kamati inayohusika na hadhi za wachezaji imekaa lini hadi katibu utoe hukumu? Tunafanya hivi vitu kufurahisha nani? Kwa interest ya kina nani? "Post a Comment

0 Comments