BETI NASI UTAJIRIKE

KUREJEA KWA DIEGO COSTA KWAIBUA MJADALA

Aliyewahi kuwa straika tegemezi kwa Chelsea Diego Costa kuna uwezekano akarejea nchini Uingereza na kuitumikia klabu yaWolver.

Costa anarejea na kusajiliwa kama mchezaji wa dharula kwa Wolves baada ya mchezaji aliyesajiliwa majira ya joto Sasa Kaljdzic na Raul jimenez kupata majeraha yatakayowaweka nje ya uwanja kwa muda  mrefu.

Sasa alisajiliwa kwa ada ya paundi milioni 15 ,kuumia kwake kunaifanya Wolves kukata rufaa kwa chama cha soka Uingereza "FA" na kuomba kufanya usajili wa dharula kisha kumuondoa Sasa kwenye kikosi chao mpaka wakati wa usajili wa majira baridi 

Diego costa anatarajiwa kuwasili viwanja vya mazoezi hapo kesho kwa ajili ya kufanyiwa majaribio na kama atafuzu basi atasajiliwa na kuanza  majukumu ndani ya timu.

Diego Costa alishawahi itumikia Chelsea kwa kiwango cha hali ya juu kwa msimu w 2014-17 akicheza michezo 89 na kufunga mabao 52.

Msimu wa 2018-2022 aliijiunga Atletico Madrid na kucheza michezo 61 na kufunga mabao 12 tu.

Msimu wa 2021 alijiunga na Atletico Mineiro alicheza mechi 15 na kufunga mabao 4.

Post a Comment

0 Comments