BETI NASI UTAJIRIKE

KOCHA SIMBA ATIMULIWA KISA YANGA

Klabu ya Simba imetangaza kuachana rasmi na aliyekuwa kocha  mkuu Zolan Maki. Kocha huyo amehudumu ndani ya Klabu ya Simba kwa siku 67 na sasa amefungashiwa vilago vyake. Simba hawajasema sababu iliyopelekea kuvunja mikataba na Zoran Maki ,kocha wa viungo Sbai Karim na kocha wa makipa Mohammed Rachid.


Zoran Maki alisaini mkataba wake na simba mwezi june na moja ya majukumu yake ni kurejesha makombe yote kwa msimu wa 2022/23 na kuhakikisha timu hiyo inafika hatua ya Nusu Fainali Michuano ya ligi ya mabingwa Afrika.

Taarifa zisizo rasmi ni kuwa Zoran Maki ameondoshwa klabuni hapo kutokana na kipigo cha bao 2-1 dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa Kombe la Ngao ya Jamii.Hivyo alishindwa kulirejesha kombe hilo na mwendelezo mbaya wa mechi za kirafiki dhidi ya Arta Solar 7 waliopoteza kwa bao 1-0 na ule dhidi ya Al Hilal waliopoteza kwa 1-0 zimekuwa ni sababu kubwa kwa Zoran kuondoshwa Simba.

Zoran Maki akiwa Simba amecheza mechi 2 za ligi kuu akifunga mabao 5 bila kufungwa bao lolote .Maki amekuwa akitumia mfumo wa 4-3-3 na mfumo huo ulifanikiwa kwa mechi mbili za awali baada ya kupiga pasi 847 huku wakipiga mashuti yaliyolenga golini 13.

Zoran Maki amehudumu katika timu 5 ndani ya miaka 5 akimiliki leseni ya UEFA Pro Licence. hizi ni timu alizofundisha Zoran Maki tangu mwaka 2017

2017–2019Primeiro de Agosto
2019–2020Wydad AC
2020–2021Al-Hilal Club
2021CR Belouizdad
2021Al-Tai
2022–Simba

Hapo kesho Simba watacheza mchezo wa ligi kuu NBC dhidi ya KMC na Suleiman Matola atakuwa kocha mkuu wa muda. Tarehe 11 timu hiyo itasafiri kuelekea Malawi  kucheza mchezo wa raundi ya kwanza Champions league dhidi ya Nyassa Big Bullets.

Hii hapa barua ya Simba 

Post a Comment

0 Comments