BETI NASI UTAJIRIKE

SIMBA NA YANGA ZIMTAFUTE FUNDI MAIKO MAPEMA

 Viongozi wa vilabu vya Simba na Yanga wanatakiwa kujitafakari haswa namna ambavyo wanaweza kuleta mabadiliko chanya ndani ya vilabu hivyo.

Simba na Yanga wamekuwa wakipata fedha nyingi kupitia udhamini, mauzo ya jezi, zawadi za michuano ya Afrika , viingilio na hata michango kutoka kwa wadau lakini mpaka leo vinategemea mechi zao zichezwe kwa mkapa.

Azam Fc walianza mwaka 2004 na leo hii wanakiwanja chao pale chamazi na wamekuwa wakitumia kwa michezo ya kimataifa na ligi nyumbani.

Kagera Sugar, Ruvu shooting na Mtibwa Sugar wanaviwanja vyao vya nyumbani japo vinachangamoto lakini walau vinawasaidia kupunguza utegemezi kutoka taasisi nyingine na wameonyesha nia ipo siku watavipanua viwanja vyao na kuwa vikubwa kama ule wa Benjamini Mkapa au ule wa Uhuru.

Namungo na Geita Gold  wao wamejiweka viwango vingine.kwa Namungo wao wamefanikwa kufikia phase ya kwanza kwa kujenga jukwaa na kuweka nyasi bandia hii inamaana msimu wa 2022/23 watacheza uwanja wa Majaliwa Stadium na watazamaji wao watakaa majukwaani kushuhudia mechi vipi kwa Simba na Yanga wenye miaka 86 

Geita Gold na wao wanajenga uwanja wao kwa style ileile ya Namungo .wako hatua ya awali kwa ujenzi wa majukwaa na kuboresha eneo la kuchezea .msimu wa 2023/24 watakuwa na uwanja wao wa nyumbani na wataachana na nyamkumbu au ccm kirumba vipi hawa Simba na yanga wanampango gani?

Kwamba wameshindwa hata kujenga jukwaa moja tu, au wameshindwa kujua hivi vilabu vidogo vinapata wapi pesa? Au na wao wanahitaji kukaguliwa hesabu zao kila mwaka ili tujue mapato na matumizi ? 

Simba na Yanga mtafuteni fundi maiko awape mbinu za kujenga viwanja tumechoka kuimba mapambio ya kila siku mara michango , mara udhamini mara uwekezaji je fedha mnapeleka wapii????

Post a Comment

0 Comments