BETI NASI UTAJIRIKE

SABABU ZA MANARA, BUMBULI KUPIGWA CHINI ZAWEKWA WAZI

 Hatimae klabu ya Yanga imetangaza rasmi kuachana na aliyekuwa afisa habari wa klabu hiyo Hassan Bumbuli. Bumbuli ameitumikia klabu ya Yanga tangu mwaka 2018 akiwa kama mkuu wa Idara ya Habari na mawasiliano wa  Klabu hiyo akishirikiana na Antonio Nugaz na baadaye Haji Manara.


Kaimu Katibu mkuu Advocate Simon Patrick amesema Bumbuli amekwishamaliza utumishi wake ndani ya Klabu ya Yanga na nafasi yake ipo wazi kwa sasa hivyo kutoa mwito kwa wadau wa soka hasa wanahabari kutuma CV zao na kuomba nafasi hiyo.

Mbali na Bumbuli kumalizana na Yanga lakini pia Haji Manara na yeye ameendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha miaka miwili kujihusisha na soka. Kitendo cha Yanga kutangaza nafasi za kazi klabuni hapo ni dhahiri Manara hana nafasi ndani ya YangaPost a Comment

0 Comments