BETI NASI UTAJIRIKE

RAGE AFUNGUKA MIPANGO YA SIMBA KWA MSIMU WA 2022/23

 Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage amefunguka kuwa msimu huu unakwenda kurudisha mataji yote waliyoyapoteza msimu uliopita.Simba imeendelea kujiimarisha kwenye eneo lake la ushambuliaji ambapo msimu huu wamekamilisha usajili wa viungo Nelson Okwa,Moses PhirimOkrah na Straika Dejan.Rage amesema usajili uliofanywa na Simba unakwenda kutibu changamoto zote zilikuwa zikiwakabili msimu uliopita. Rage amenukuliwa akisema

"Msimu uliopita haukuwa bora upande wetu,hii inatokana na aina ya usajili ambao tulifanya ,wachezaji wengi walishindwa kutupa kile ambacho tulitarajia huku wengihne wakiandamwa na majeraha ya mara kwa mara "

"Msimu huu viongozi wetu wamejua wapi tuliteleza na aina ya usajili uliofanywa ni wazi tunakwenda kuwa tishio,wachezaji waliosajiliwa msimu huu wote ni wazuri na nina uhakika tunakwenda kurudisha makombe yetu yote ambayo watani wetu Yanga wameyatwaa msimu uliopita,wachezaji wanapaswa kutambua kuwa wanadeni kubwa kwa mashabiki ,hivyo wanatakiwa kupambamna katika mechi zote watakazocheza iwe nyumbani au kimataifa"

Post a Comment

0 Comments