BETI NASI UTAJIRIKE

NYOTA WAWILI KUTUA NDANI YA CHELSEA KABLA YA DIRISHA KUFUNGWA

 Zikiwa zimesalia siku 20 ili kufungwa kwa dirisha la usajili la Ulaya klabu ya Chelsea inaendelea kuongeza nguvu kwenye kikosi chake na wakati huu wanawinda saini ya nyota wawili akiwemo Frank De Jong na Pierre Aubemayang. 


Barcelona mpaka sasa wamekwishatumia zaidi ya Euro milioni 140 kuwasaini nyota watano akiwemo Roberto Lewandowski na rafinha hivyo kuendelea kukuza deni la klabu na kufikia kiasi cha Euro bilioni 1.14. La Liga chama cha soka cha Hispania kimeitaka klabu hiyo kuonyesha namna ambavyo kitawalipa wachezaji wake na wanatakiwa kuwa na zaidi ya paundi milioni 85 kwenye akaunti yao.

Shinikizo la La Liga linaifanya Barcelona ilazimike kuwauza wachezaji hao ikiwemo De Jong ambaye kila mwaka hupokea euro milioni 17 kama mshahara na amekataa kupunguza mshahara huo. manchester United walimuwinda nyota huyo kwa muda mrefu lakini walishindwa kumnunua.Chelsea wao wameanza harakati za kutaka kumsajili kiungo huyo na kama atatua klabuni hapo basi Barcelona wataepukana na rungu la La Liga .

Mpaka sasa Chelsea imefanikiwa kuwanasa nyota kadhaa akiwemo Beki wa kushoto Marc Cucurela,Winga Raheem Sterling beki wa kati Koulibary hivyo watamuhitaji Pierre Aubemayang aimarishe nafasi ya Ushambuliaji huku De Jong akiimarisha nafasi ya Kiungo.

Nafasi ya De Jong ndani ya Barcelona itachukuliwa na Benardo Silva anayewindwa na klabu hiyo na thamani ya mchezaji huyo ni paundi milioni 80 kama Manchester City watamuuza.

Post a Comment

0 Comments