Wadau mbali mbali wameionya klabu ya Manchester City kuhusiana na suala la kutaka kumuuza kiungo mshambuliaji Bernado Silva anayewaniwa na Barcelona. Mchambuzi mkongwe wa soka na mchezaji wa zamani wa Chelsea Jason Cundy amenuikuliwa akisema hayo baada ya tetesi kuenea kwamba Manchester City wameamua kumuweka mchezaji huyo sokoni kwa dau la paundi milioni 80 huku Barcelona wakimuwania.
Jason Cundy amenukuliwa akisema
"Hakuna namna Bernardo Silva anaweza kuondoka nyakati za dirisha hili,Kuna wakati Guardiola alisema hadhani kama Bernado anaweza kubakia kwenye klabu ,kuna uwezakano wakamruhusu aweze kuondoka lakini sidhani kama itawezekana"
"Itanishangaza kama wataruhusu Bernado Silva aondoke ,waliwekeza kwa Grealish kiasi cha paundi milion 100 lakini tukashuhudia jinsi walivyoshindwa kufanya vizuri kwenye michhuano ya Champions ligi ,Unapomuondoa Silva unazidi kudhoofisha kikosi chako na hata Watu wa Liverpool watakuwa na kazi nyepesi sana kukuletea upinzani "
"Maisha ya Manchester City yatakuwa magumu bila Bernardo Silva" Alimaliza kwa kusema Bwana Jason Cundy
0 Comments