BETI NASI UTAJIRIKE

MAMA MZAZI AWEKA NGUMU KWA MANCHESTER UNITED

 Manchester United wameendelea kupata wakati mgumu kumsajili Adrien Rabbiot.Taarifa za ndani zinasema Manchester United na klabu yake ya Juventus wamekwisha kubaliana na wanaelekea kumalizana lakini Mama mzazi wa nyota huyu ameonekana kuleta zengwe kwa Manchester United akitaka nyota huyo alipwe fedha nyingi za mshahara.


Adrien Rabbiot akiwa Juventus amekuwa akilipwa paundi milioni 6 kwa Mwaka na mama mzazi ambaye ni meneja Veronique Rabbiot ameonekana kuweka msimamo mkali kuhusu maslahi na kama Man U watashindwa kutoa pesa wanazozitaka  basi nyota huyo hatatua old Trafford

Mfahamu Adrien Rabbiot

Adrien Rabbiot alizaliwa mwaka 1995 huko Ufarana na mwaka 2012-14 alianza kuitumikia Paris Saint Germain B na baadaye akapandishwa timu ya wakubwa PSG senior team mpaka mwaka 2019 alipouzwa kwenda Juventus.

Kiungo huyo ameitumikia Juventus kwa mafanikio makubwa akiisaidia timu hiyo kutwaa kombe la Serie A na Copa Italy .kwa upande wa timu ya taifa Rabiot alikuwa ni moja ya nyota waliobeba kombe la dunia mwaka 2018 nchini Qatar naUefa Euro 2020.

Kama atatua Manchester United atakwenda kuongeza nguvu kwenye eneo la kiungo.

Post a Comment

0 Comments