BETI NASI UTAJIRIKE

VITA YA URUSI NA UKREINI YACHOCHEA MAPAMBANO KWA WACHEZAJI

 Timu ya taifa Ukreini usiku wa jana ilikuwa na wakati mzuri baada ya kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Scotland mchezo wa kufuzu kombe la dunia Qatar 2022.Magoli ya Ukraini yalifungwa na Andriy Yarmolenko dakika ya 33,roman yaremchuk dakik ya 49 na Artem Dovbyk dakika ya 90 huku bao pekee la Scotland likifungwa na McGregor dakika ya 79.

Matokeo hayo yanaifanya Ukreini kuingia hatua inayofuata kucheza na Wales na kama watashinda mchezo huo basi wataelekea fainali za kombe la dunia nchini Qatar kwa mwaka 2022.

Ushindi huu umekuwa faraja kwa raia wa Ukreini hasa baada ya nchi yao kuvamiwa na Urusi na kusababisha maelfu ya watu kukimbia nchi hiyo huku wengine wakiuawa kutokana na vita hiyo. 

Mchezaji wa Manchester City Oleksandr Zinchenko alinukuliwa kabla ya mchezo  akisema " nilazima tushinde mchezo huu mgumu ili kurejesha furaha kwa mashabiki wetu" 

Post a Comment

0 Comments