Mkurugenzi mtendaji wa Klabu ya Yanga Senzo Mazingisa amezungumzia kwa ufupi suala la mikataba kwa nyota wake ndani ya klabu ya Yanga.Senzo amewataja Yannick Bangala na Juma Shabani kwamba wapo kwenye mazungumzo ya kuwabakisha nyota hao.
Nyota hao ambao wamekuwa na msimu mzuri wakiisaidia klabu hiyo kutwaa mataji mawili ikiwemo ligi kuu na Ngao ya jamii. Wachezaji hao wamekuwa wakitegemewa na klabu hiyo na sasa wamebakiwa na miezi 12 ili mikataba yao iweze kumalizika .
Yanga bado inawahitaji wachezaji hao na sasa wanapambana wawezavyo kuwabakisha klabuni hapo kuelekea msimu ujao ikizingatiwa watashiriki michuano ya ligi ya mabingwa Africa.Nyota hao wana uzoefu mkubwa na michuano hiyo baada ya kucheza walipokuwa AS Vita.
Mbali na nyota hao jina la Fiston Mayele lilitajwa na vilabu vya RS Berkane na Kaizer Chief wakihitaji kumnunua lakini Senzo alinukuliwa akisema
"Tuna malengo ya kufanya vizuri ligi ya mabingwa msimu ujao hivyo hatuwezi kuwauza wachezaji wetu muhimu. Kupata fedha ni jambo moja lakini kuwaheshimu mashabiki ni jambo jingine.kama tukimuuza mayele tutawaeleza nini mashabiki?"
0 Comments