BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA YAWAUMBUA WASIOITAKIA MAFANIKIO KLABU YAO

Wakati Yanga wanaendelea kusherehekea ubingwa wao wa 28 ligi kuu ,wadau wa soka na Mashabiki mbali mbali walihoji kuhusiana na picha za kocha mkuu wa klabu hiyo Nabi pamoja na mwenyekiti Mshindo Msolla. Baadhi ya wachambuzi walidai Protokali haikuzingatiwa na klabu ya Yanga hasa baada ya wawili hao kutoonekana  wakiwa na picha za kombe na baadhi walifika mbali kwa kusema tukio la kutokuwepo kwa picha za watu hao ni kudharau mchango wao ndani ya timu hiyo.

Leo hii Klabu ya Yanga imetoa picha za DKT Mshindo Msola pamoja na Kocha Nabi wakiwa na kombe hilo na kufuta sintofahamu iliyojitokeza.Hizi hapa ni baadhi ya picha Post a Comment

0 Comments