BETI NASI UTAJIRIKE

MESSI AWEKA REKODI MPYA ARGENTINA IKITWAA KOMBE

 Hatimaye Lionel Messi ameweka rekodi mpya kwa timu yake ya taifa baada ya timu hiyo kushinda mabao 3-0 dhidi ya Italy kwenye kombe la Finallisima

Kwenye mchezo huo Lionel Messi alitengeneza mabao mawili yaliyofungwa na Laurato Martinez pamoja na Paulo Dybala huku bao jingine likifungwa na Angel Di Maria akitengewa na Laurato Martinez.

Hili linakuwa kombe la pili kwa Lionel Messi akitwaa ndani ya timu ya taifa Argentina . Mwaka 2021 Messi aliiwezesha Argentina kutwaa Copa America na yeye kuibuka mchezaji bora na mfungaji bora wa michuano hiyo na ushindi huo ukapelekea yeye kuweza kushiriki michuano ya finallisima inayozikutanisha timu bingwa kwa bala la ulaya na America kusini ( CONMEBEL-UEFA CHAMPIONS) Ambapo kwa upande wa ulaya ITALY ndiye alikuwa bingwa.

Historia kwa Ufupi 

Michuano hii ilianzishwa mwaka 1985 na timu ya taifa ufaransa ilitwaa kombe hilo dhidi ya Uruguay. Mwaka 1993 Argentina ilitwaa kombe hilo dhidi ya Denmark na kwa wakati huo Diego Maradona akielekea kumaliza soka lake. Michuano hiyo ilisimama kwa miaka 29 bila kuchezwa na mwaka 2021 uefa na conmebol ziliamua kurejesha michuano hiyo iliyopigwa dimba la Wembley nchini Uingereza.Post a Comment

0 Comments