BETI NASI UTAJIRIKE

MBEYA CITY YAZIDI KUPOTEZA MATUMAINI YA RUVU SHOOTING LIGI KUU

 Klabu ya Mbeya City imezidi kufifisha matumaini ya klabu ya Ruvu Shooting kusalia ligi kuu NBC kwa msimu wa 2022/23 baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1 lililofungwa na Baraka Mwalubunju dakika ya 67 na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa Mbeya City 1-0 Ruvu Shooting.Matokeo hayo yanawafanya Mbeya City kufikisha pointi 35 kwenye michezo 28 waliyocheza pointi sawa na kagera sugar aliye nafasi ya 8. Kama Mbeya City atashinda michezo yake dhidi ya Yanga na Namungo basi atafikisha pointi 41 na kumweka nafasi bora zaidi kwenye msimamo wa ligi.

Kipigo hicho kinawafanya Ruvu shooting wasalie nafasi ya 13 wakiwa na pointi 28 kwenye michezo 28 waliyocheza huku wakishindwa kupata ushindi kwenye mechi 5 mfululizo za ligi kuu . Ikumbukwe Ruvu Shooting alipata ushindi wake wa mwisho Mei 12 dhidi ya Geita Gold na baada ya hapo alipata sare dhidi ya KMC,KAGERA SUGAR,AZAM na kupigwa mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Matokeo hayo mabovu yanamfanya kocha Mkwasa kuwa na wakati mgumu akiwa na mechi mbili ngumu mkononi dhidi ya Mbeya Kwanza anayeshikilia mkia na Tanzania Prisons aliyenafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi kuu huku timu hizo zikipambana kujinasua na pigo la kushuka daraja.

Kama Ruvu Shooting atapoteza michezo hiyo basi kuna uwezekano wa kushuka daraja moja kwa moja 


Post a Comment

0 Comments