BETI NASI UTAJIRIKE

MBADALA WA MO SALAH NA MANE APATIKANA LIVERPOOL

 Klabu ya Liverpool imeendelea kujipanga kuelekea msimu ujao hasa eneo la usajili baada ya nyota wake wanne wa kikosi cha kwanza kutaka kuondoka klabuni hapo.


Mohammed Salah mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu wa 2022 /23 na mpaka sasa hajasaini kandarasi mpya huku Sadio Mane akiwekwa sokoni kwa dau la paundi milioni 30 na Bayern wakitajwa kumuhitaji.

Roberto Firmino amekuwa na kiwango cha kusuasua kwa misimu miwili na sasa anajiandaa kuachana na Liverpool. Kiungo Origi amekwishaangwa na klabu hiyo na sasa ni mchezaji huru kujiunga na klabu yoyote.

Wasifu wa Mchezaji Mpya 

Darwin Nunez raia wa uruguay anayekipiga klabu ya Benfica anatajwa kurithi mikoba ya nyota hao wanne ndani ya Liverpool. Mpaka sasa mchezaji huyo amecheza michezo 38 ya michuano mbalimbali ngazi ya klabu akifunga mabao 32.

Kuwasili kwa Nunez kutaifanya safu ya ushambuliaji Liverpool kuwa moto mkali zaidi kwani itaongozwa na vijana wadogo akiwamo Luis Diaz, Diogo Jota, Minamino na sasa Nunez. 

Taarifa za ndani zinasema klabu ya Liverpool imejihakikishia kumnasa nyota huyo na wameshaanza mazungumzo na mawakala pampja na uongozi wa Benfica


Post a Comment

0 Comments