BETI NASI UTAJIRIKE

MASHABIKI WAIVAMIA SIMBA IKIWASILI SONGEA

 Klabu ya Simba imewasili mjini Songea kupambana na Mbeya KWanza mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara utakaopigwa dimba la Majimaji Songea tarehe 29 mwezi huu. Simba wamewasili Songea mchana wa leo wakitokea Mbeya baada ya kumaliza mchezo wake wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons mchezo uliomalizika kwa Prisons kupata ushindi wa bao 1-0.


Mchezo huu wa mwisho kwa msimu huu unaifanya klabu ya Simba kushindwa kutwaa taji lolote la ndani kwa msimu huu wakimaliza msimu nafasi ya pili wakiwa na tofauti ya pointi 11 nyuma ya Bingwa Yanga. Kwa upande wa Mbeya Kwanza wao watakuwa wanaaga ligi kuu Tanzania Bara baada ya kushindwa kufanya vizuri kwa msimu huu.

Mbali na kutokuwa na msimu mzuri lakini hiyo haikuwazuia mashabiki wa Simba Songea kuonyesha mapenzi kwa kuvamia hoteli waliyofikia wachezaji na walikuwa wakiwashangilia kwa makofi na nyimbo.

Hizi ni baadhi ya picha za nyota hao wakiwasili Songea na namna walivyopokelewa












Post a Comment

0 Comments