BETI NASI UTAJIRIKE

BAADA YA DILI LA ARSENAL,CHELSEA KUKAA SAWA GABRIEL JESUS AIBUKA KIVINGINE

 Mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus ameendelea kuwa na furaha kwa mara nyingine baada ya kufanikiwa kupata mtoto wake wa pili.Hili linakuwa ni tukio lake la pili ndani ya mwezi huu baada ya lile la kwanza kuhusishwa kujiunga na Arsenal au Chelsea majira haya ya joto.

Nyota huyo wa brazil amekuwa na kiwango kizuri ndani ya Manchester City kwa msimu huu akiisaidia kutwaa taji la ligi kuu Uingereza lakini ameingiwa na wasiwasi wa kuwa chaguo la kwanza mbele ya Eerling Haaland aliyesajiliwa msimu huu.

Manchester City wamemweka sokoni na dau lake ni paundi milioni 40. Ikumbukwe nyota huyu alianza soka lake nchini Brazil na aliitumikia klabu ya Palmeiras kwa msimu wa 2015-17 kisha kununuliwa na Manchester City alikocheza mechi 159 na kufunga mabao 56.

Post a Comment

0 Comments