BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO ALHAMIS TAREHE 07-04-2022

 Liverpool inamtaka winga wa Villarreal na Uholanzi Arnaut Danjuma, 25, kuchukua nafasi ya mshambuliaji Sadio Mane, lakini Liverpool haina mpango huo kwa sasa hadi mwaka 2023. (Goal)Kama kocha wa Ajax Erik ten Hag akichaguliwa kuwa meneja wa Manchester United kama invyotarajiwa, basi atamsajili kiungo wa kati wa Portugal Ruben Neves, 25, Kutoka Wolves. (Sun)Mholanzi Ten Hag anamtaka pia beki wa Ajax na Jurrien Timber aende naye Old Trafford. (Star)

Wakala wa mchezaji wa Chelsea na Ujerumani Timo Werner, 26, yupo nchini Italia akikutana na AC Milan, Juventus na Atalanta . (Corriere dello Sport - in Italian)

Paul Pogba , 29, anapendelea kurudi Juventus kuliko kwenda Paris St-Germain baada ya muda wake kuisha majira ya joto. Lakini kwa upande wa Italia wana wasiwasi kuhusu pesa anazotaka kulinganisha na umri wake (Tuttosport - in Italian)

Arsenal, Everton na Newcastle wote wameonesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Uholanzi Memphis Depay kutoka Barcelona. (Superdeporte - in Spanish)

Winga wa PSV Eindhoven na Uholanzi Cody Gakpo, 22, ameweka wazi mapenzi yake kwa Arsenal huku akiendelea kuunganishwa na wenyeji wa vilabu vingine ikiwemo Manchester United na Liverpool. (Goal)

M

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Viongozi wa ngazi za juu huko Inter Milan sasa wanataka mshambuliaji wa Chelsea na Belgium Romelu Lukaku (28) arudi klabuni hapo. (Mirror)

Leicester City wameonesha nia ya kumtaka mlinzi wa FC Mainz's Jeremiah St. Juste, 25. (Bild - via Leicester Mercury)

Brighton hawana mpango wa kumuuza kipa wake Sanchez mbali ya kuwa Newcastle wameonesha nia ya kumuhitaji kipa huyo Mhispania (24). (Football Insider)

L

Barcelona ina Imani kuwa ina nafasi kubwa ya kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski, 33, msimu huu wa majira ya joto. (Sport - in Spanish)

Kiungo wa kati wa Ajax na Uholanzi Ryan Gravenberch, 19, amekubali kuingia mkataba binafsi na Bayern Munich. (Bild - via Bundesliga News)

W

CHANZO CHA PICHA,AFP

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 23, anaweza kutia Saini mkataba mpya katika klabu yake ya Paris St-Germain mbali na kuonesha nia kwa Real Madrid. (Sky Sports)

Mlinzi wa Leeds Luke Ayling, 30, amesema kuwa anataka kumalizia muda wake katika soka kama mchezaji katika klabu hiyo. (Star)

Post a Comment

0 Comments