BETI NASI UTAJIRIKE

SIMBA YAJIPANGA KUINGIA KIMAFIA AFRIKA KUSINI

 Klabu ya Simba inalazimika kuingia kimafia nchini Afrika Kusini ili kuwachanganya wapinzani wao Orlando Pirates. Klabu hizo zitamenyana siku ya jumapili kwenye mchezo wa pili wa robo fainali baada ya ule wa kwanza kumalizika jijini Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0.


Mpaka sasa wachezaji wa klabu hiyo hawajaondoka jijini Dar es Salaam na bado haijafahamika ni lini wataondoka ilihali mchezo wao utapigwa tarehe 24 . Mkurugenzi mkuu wa klabu Barbara Gonzalez  amekwisha wasili nchini Afrika ya kusini akiwa na baadhi ya viongozi wa timu hiyo kwa ajili ya maandalizi ya awali.

Mara baada ya kuwasili nchini humo walipokelewa na balozi wa Tanzania nchini humo na walipeleka ombi la ulinzi kwa wachezaji mara tu baada ya kuwasili nchini humo. Uongozi wa Simba umefikia hatua hiyo baada ya kocha wa Orlando Pirates kutoa kauli za vitisho kwa klabu hiyo itakapowasili Afrika Kusini.

Kuna uwezekano wachezaji wa Simba wakaondoka kwa mafungu mafungu kuelekea Afrika Kusini ili kuwachanga wapinzani wao lakini pia wanaweza kuondoka siku ya jumapili Asubuhi na kuingia uwanjani jioni

Post a Comment

0 Comments