BETI NASI UTAJIRIKE

KARIM BENZEMA AVUNJA REKODI YA CRISTIANO RONALDO

Karim benzema ameingia kwenye vitabu vya kihistoria usiku wa jana baada ya kufunga mabao matatu dhidi y Chelsea kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya hatua ya robo fainali.

Benzema anakuwa mchezaji wa pili kufunga mabao matatu kwa michezo miwili mfululizo akifanya hivyo dhidi ya PSG kwenye hatua ya 16 bora ambapo Real Madrid walishinda mabao 3-1 na mchezo wa robo fainali dhidi ya chelsea raundi ya kwanza robo fainali kwa kufunga mabao matatu.

Cristiano Ronaldo ndiye aliyekuwa anashikilia rekodi hiyo baada ya kuwafunga Bayern Munich na Atletico Madrid hat trick kwenye hatua ya 16 bora na robo fainali za michuano hiyo.

Benzema kwa sasa amefikisha jumla ya mabao 36 kwa msimu wa 2021/22 na hii ni mara ya kwanza kwa mshambuliaji kufikisha idadi ya mabao hayo tangu alipojiunga na Real Madrid. Benzema pia amefikisha mabao 82 ya ligi ya mabingwa ulaya akishika nafasi ya nne nyuma ya Lewandowski.

Kwa msimu wa 2021/22 Benzema amefunga mabao 10 kwenye mechi 9 alizocheza huku anayeongoza orodha hiyo ni Lewandowski mwenye mabao 12 kwenye michezo 9 aliyocheza

Orodha ya wafungaji bora Uefa tangu kuanzishwa kwake

1. Cristiano Ronaldo mabao 142
2.Lionel Messi mabao 125
3.Robert Lewandowski mabao 85
4.Karim Benzema mabao 82
5.Raul Gonzalez mabao 71

Post a Comment

0 Comments