BETI NASI UTAJIRIKE

JUVENTUS YAFUZU FAINALI ZA COPPA ITALIA TENA

 Juventus imefanikiwa kuingia tena fainali za michuano ya Coppa Italia baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fiolentina. Juventus watakutana na Intermilan mchezo wa fainali uliopangwa kufanyika Mei 11.

Mabao ya Juventus yalifungwa na Bernadesh dakika ya 32 huku kiungo mbrazil Danilo wakifunga bao la pili dakika ya 90 ya mchezo. Inter Milan aliingia fainali za michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya mpinzani wake wa jadi AC Milan.

Historia Fupi ya michuano

Michuano hii ilianzishwa mwaka 1922 na mwaka 2022 inatimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwake. Bingwa mtetezi ni Juventus na ndiye mwenye makombe mengi zaidi akishinda mara 14.

Post a Comment

0 Comments