BETI NASI UTAJIRIKE

KOCHA MPYA AFUNGUKA BAADA YA KUTUA MANCHESTER UNITED

 Hatimaye klabu ya Manchester United imefanikiwa kumpa kandarasi ya miaka mitatu kocha Erik Ten Hag.Kocha huyo amepewa mkataba wa miaka mitatu na kazi rasmi ataanza mwanzoni mwa msimu wa 2022/23.


Tag ametua Manchester United akitokea Ajax ya Netherlands na ataitumikia klabu hiyo mpaka june mwaka 2025 kukiwa na kipengere cha kuongeza mkataba wa miaka mingine kama atashinda mchezo huo.

Baada ya kusainishwa mkataba huo Tag amenukuliwa

 "Hii ni fursa ya kipekee kuwa meneja  Manchester United,nina furaha sana kuteuliwa.

Ninajua historia ya klabu hii kubwa na jinsi mashabiki wake wanavyoipigania,ninajipanga kufanya tathimini ya namna  ninavyoweza kuleta mafanikio yanayostahili"

"Ni ngumu sana kuondoka Ajax baada ya muda nyakati nzuri lakini nawahakikishia mashabiki wa Manchester United kuwa msimu wa 2022/23 tutakuwa vizuri zaidi "

Post a Comment

0 Comments