BETI NASI UTAJIRIKE

CHELSEA,TOTENHAM SAFI MAN UNITED NA ARSENAL ZALALA YOO

 Klabu ya Chelsea imeendelea kusalia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza baada ya ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Southampton. Chelsea wamefikisha pointi 62 kwenye michezo 31 waliyocheza mpaka sasa.

Totenham Hotspurs wamesalia nafasi ya 4 baada ya kujipatia ushindi mnono mabao 4-0 dhidi ya Aston villa mchezo uliopigwa dimba la villa park. Ushindi huo unaifanya TOttenham kufikisha point 57 kwenye michezo 31 waliyocheza.

Arsenal imeshindwa kabisa kurudi nafasi ya nne baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Brightons.kipigo hicho kimeifanya Arsenal kusalia nafasi ya 5 ikiwa na pointi 54 baada ya michezo 30 ya ligi

Manchester United imezidi kupoteza matumaini kwa mashabiki wake baada ya kuambulia kipigo kingine kutoka kwa Everton na kuifanya iporomoke mpaka nafasi ya 7 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 51 kwenye michezo 31 waliyocheza.

Post a Comment

0 Comments