BETI NASI UTAJIRIKE

MCHAMBUZI AWACHANA WANAOBEZA MAENDELEO YA SIMBA NA YANGA KIMATAIFA

 Ameandika Farhan Kihamu -

Walichofaulu sana Waingereza sio tu uwekezaji wa ndani ya uwanja ila ni uzalendo wao kama taifa, tunaweza kusema mengi ila suala linapokuja timu ya England kwenye soka la Ulaya basi ni jambo lao wote kama nchi

Sahau kuhusu vita zamani taifa lilikuwa linasifika kisa vita (Millitary Supremacy) achana na kuhusu uchumi tayari mambo ya G8 mpaka G20 sio stori sana, sasa hivi mpira ni suala la NATIONAL PRESTIGE, kama taifa linaungana

Juzi wakati Liverpool, Manchester City, West Ham, Leicester City na Rangers wanafuzu hatua zinazofuata kwenye michuano ya Ulaya basi hashtag mitandaoni ilikuwa BREXIT BOYS RULLING EUROPE! Yes ni ufahari kwa visiwa vyote vya Uingereza

Sahau kuhusu uhasama wa Mersysides, sahau kuhusu uhasama wa Midlands au North East Rivarly, sahau kuhusu Glasgow Derby, wao suala la taifa lao ni suala lao wote! Media zao, Wachambuzi wao wanazipa nguvu timu zao

Hata Waarabu hapa Afrika wanafanikiwa kutokana na neno ARAB NATIONALISM, Yes! Ahly anapokuwa na jambo lake ile Cairo ipo kimya kupisha jambo la Mashetani, kule Morocco pia linapokuja suala lao ni wao 

Yes! Mkifika Cairo kutoka huku Kusini mwa Jangwa la Sahara mnaulizwa swali “MMETOKA AFRIKA?” Yes wapo sahihi, huku kwetu tuna uswahili mwingi sana, hatumpi nafasi aliyejuu aendelee kuwa juu, tunataka wote tushuke tuchekane, hiyo ndio mentality yetu

Leo hii ukienda kusoma comments za Wasauzi kuhusu mechi ya jana kwa utafiti wangu ni 98%  wote Wasauzi wapo nyuma ya Pirates, wanamaanisha utaifa wao na ufahari wao! Ndio maana halisi ya utaifa

Huku kwetu Simba wakati mwingine anapigwa vita, mpinzani anasaidiwa kupewa nguvu, lakini tunasahau hizi ni mechi za Afrika kwa ajili ya kuweka ramani, ile agenda ya VISIT TANZANIA ni kwa ajili ya hospital kule Longido, Shule kule Morogoro na madaraja kule Tukuyu

Sio suala la Simba ni suala la taifa, chuki ni mzigo mkubwa usiubebe! Please dont!

THE YOUNG DIGALA

VISIT MOROGORO🇹🇿

Post a Comment

0 Comments