Michuano ya Uefa Europa League ama kama wanavyosema UEFA ndogo inaendelea leo usiku kwa hatua ya robo fainali kwa hatua ya nusu fainali ambapo miamba mbali mbali itachuana usiku huu.
Barcelona chini ya kocha Xavi Hernandez itakuwa ugenini dhidi ya Frankfurt mchezo utakaopigwa nchini Ujerumani. Mchezaji anayetegemewa kufanya makubwa zaidi ni Pierre Aubemayang kutokana kuwa na rekodi nzuri kwa msimu huu tangu alipojiunga na barcelona.
Mchezaji huyu anarekodi ya mabao 24 yasiyo ya penati i kwenye michuano hiyo kwa kuwa na jumla ya magoli 24 aliyofunga akiwa Arsenal ,Borrusia Dortmund na sasa Barcelona rekodi inayoshikiliwa na Radamel Falcao mwenye mabao 27 yasiyo ya Penati.
Hizi hapa ni mechi zitakazopigwa usiku wa leo na marudio yake ni tarehe 14 april.michuano hii itamalizika tarehe 18 mei 2022
0 Comments