BETI NASI UTAJIRIKE

STERLING APIGA HAT TRICK MANCITY IKIZIDI KUPAA KILELENI

 KLabu ya Manchester City imezidi kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi kuu baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Norwich mchezo uliopigwa dimba la Carrow Road.


Manchester City walijipatia bao la kwanza dakika ya 31 kupitia Raheem Sterling dakika ya 31 na mchezaji huyo alifunga bao la tatu dakika ya 70 na huku akikosa penati dakika ya 90 na kufunga dakika ya 91 kwenye mchezo huo. Phil Foden naye ameendelea kuonyesha uwezo baada ya kufunga bao la pili dakika ya 48 ya mchezo.

Matokeo hayo yanawafanya Manchester City wajikite kileleni wakiwa na pointi 63 baada ya michezo 25 huku Liverpool wakiwa nafasi ya 2 wakiwa na pointi 51 baada ya michezo 23.

Post a Comment

0 Comments