BETI NASI UTAJIRIKE

MAN UNITED YAZIDI KUTIBUA MASHABIKI WAKE

 Mashabiki wa Manchester United wameendelea kuugulia maumivu wikiendi hii baada ya timu hiyo kutoka sare na Southhampton kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza.Huu unakuwa ni mchezo wa tatu mfululizo kwa klabu hiyo kushindwa kupata ushindi .


Mara ya mwisho klabu hiyo kupata ushindi ni dhidi ya Westham kwenye mchezo uliomalizika kwa United kushinda kwa bao 1-0 .Timu hiyo inayonolewa na Ralf Rangnick iliondolewa kwenye kombe la FA baada ya kufungwa na Middlesbrough.

February 8 Man U ilitoka sare ya kufungana 1-1 na Burnley na tarehe 12 february imetoka sare ya 1-1 dhidi ya Southhampton wakifikisha pointi 40 baada ya michezo 24 na kukaa nafasi ya 5.Mashabiki wa Manchester United wanahali mbaya kutokana na ratiba ngumu waliyonayo kwa mwezi Machi na April ilihali timu hiyo haijatengamaa.

Klabu hiyo imekuwa na changamoto kwa eneo la ushambuliaji mbali na kuwa na wachezaji mahili kama Cristiano Ronaldo,Edison Cavan,Rashford ,Martial,Sancho ,Bruno na Lingard.Huku eneo la ulinzi likiwa tatizo mbali na uwepo wa mabeki wazoefu akiwemo Kapteni Harry Maguire,Varane ,Jones,Baily na Lindelof wakishindwa kuzuia washambuliaji mbalimbali na kumpa wakati mgumu David De Gea 

Ratiba ya Manchester United kwa mechi  6 zijazo

1.Manchester United vs Manchester City

2.Manchester United vs Tottenham

3.Manchester United vs Atletico Madrid

4.Liverpool vs Manchester United

5.Manchester United vs Leicester City

6. Everton vs Manchester United 

Post a Comment

0 Comments