BETI NASI UTAJIRIKE

HATIMAYE CHELSEA YAFIKIA REKODI YA MANCHESTER UNITED NA LIVERPOOL

 Baada ya kusubiri kwa takribani miaka 22 tangu kuanzishwa kwa michuano ya FIFA CLUB WORLD CUP hatimaye mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa ulaya Chelsea wamefanikiwa kutwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza.Mchezo huo mkali uliopigwa dimba la The Mohammed Bin Zayed Stadium Abu Dhabi uliwafanya Chelsea kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Palmerais ,Shukrani za dhati zimwendee Romelu Lukaku aliyewapa bao la uongozi dakika ya 55 ya mchezo wao dhidi ya Palmeras na bao la ushindi likiwekwa kimiani na Kai Havert dakika ya 117 kwa mkwaju wa penati na kuifanya Chelsea kuungana na Manchester United na Liverpool kutwaa kombe hilo.

Klabu ya Chelsea imefanikiwa kucheza fanali za michuano hiyo kwa mara ya pili. fainali ya kwanza walicheza dhidi ya Corinthians ya nchini Brazil nawalipoteza kwa bao 1-0 mwaka 2012. Miaka 10 baadaye wamefanikiwa kulipa kisasi kwa kuwafunga Palmeiras ya nchini Brazil

Real Madrid ndiyo klabu inayoongoza kwa mataji ya Fifa Club World Cup ikitwaa mara 4 mwaka 2014,2016,2017,2018,Barcelona ikitwaa mara 3 mwaka 2009,2011 na 2015 ,Bayern Munich imetwaa mara mbili mwaka 2013 na 2020 ,AC Milan mwaka 2007,Inter Milan mwaka 2010 ,Liverpool mwaka 2019 ,Chelsea mwaka 2021 na Manchester United mwaka 2008.

Kwa vilabu vinavyotoka mabara mengine tofauti na Ulaya na kutwaa ubingwa huo ni Corianthians mwaka 2000 na 2012,Internacional 2006,Sao Paulo 2005 zote kutoka Amerika ya kusini na nchini Brazil


Post a Comment

0 Comments