BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA YAJA KIMAFIA ZAIDI YAWAVURUGA WAPINZANI MAPINDUZI CUP

 Klabu ya Yanga imeamua kufanya maamuzi ya kuwavuruga wapinzani wao kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar baada ya kukaa kimya tangu michuano hiyo ilipoanza january 2.


Mpaka sasa haijulikani kuwa Yanga wapo jijini Dar es salaam ama wameshawasili Zanzibar. Swali hilo limeibuka baada ya ukimya kuanzia kwa viongozi na wachezaji kutoweka picha mahali popote kama  vilabu vya Simba ,Azam na Namungo vilivyofanya wakati vikiondoka Dar es salaam,vikiwasili Zanzibar na hata mazoezini.

Kwa upande mwingine wachezaji wa kikosi cha kwanza takribani 6 hawamo katika msafara huo,kocha nabi na kocha msaidizi Kaze na wao wako nje ya nchi.Swali linakuja je Yanga wako wapi? wameingia zanzibar kimafia? ama wameamua kuijibu simba juu ya ufichaji taarifa.

Haji Manara na Hassan Bumbuli wao pia wamekaa kimya na hata mitandao ya kijamii ya Yanga haijaandika chochote mpaka sasa, mashabiki wa timu  hiyo hawaelewi ni wapi walipo wachezaji wao huku wapinzani wao wakichanganyikiwa zaidi 

Post a Comment

0 Comments