BETI NASI UTAJIRIKE

JE SHAIBOB NI CHAGUO SAHIHI LA PABLO AU VIONGOZI WA SIMBA WAMEKURUPUKA

 Klabu ya Simba imemrejesha kundini mchezaji wake wa zamani Sharaf Eldin Shaibob aliyeitumikia klabu hiyo msimu wa 2019/20


mbali na kuwa na kiwango kizuri kwa msimu huo lakini Shaiboub hakuwa na namba ya uhakika wa namba kwa msimu huo kutokana na utitili wa viungo wengi mno ndani ya klabu hiyo ambapo alolitimkia Cs Constantine ambako nako hakucheza mchezo hata mmoja. 

Kwa sasa Shaiboub amerejea Msimbazi kwa majaribio kipindi hiki cha dirisha dogo na kama atafuzu kwenye michezo ya kombe la Mapinduzi basi atajumuishwa ndani ya kikosi cha Simba kwa msimu wa 2021/22

Mwalimu Pablo ameonekana kutopata kile anachokitafuta hivyo uwepo wa Shaibob unaweza kumrahisishia kazi yake kuelekea michuano ya ligi kuu, fa pamoja na kombe la shirikisho.

MaShabiki wanahoji je ni nani haswa anafaa kusajiliwa na kuachwa na klabu ya Simba hasa kwa wageni walishindwa kuonyesha umakini walipopata nafasi. Na je mwalimu Pablo alionyeshwa kanda za video za Shaiboub ama viongozi wameamua kumrejesha kinguvu.

Post a Comment

0 Comments