Michuano ya 33 ya Kombe la Mataifa ya Afrika inaanza nchini Cameroon Januari 9 Jumapili, ikiwa imecheleweshwa kwa mwaka mmoja kutokana na janga la corona.
Hapa, tunaangazia kundi A, ambalo linajumuisha wenyeji Cameroon, Burkina Faso, Ethiopia na Cape Verde.
Ratiba
Jumapili 9 Januari: Cameroon v Burkina Faso, Ethiopia v Cape Verde
Alhamisi 13 Januari: Cameroon v Ethiopia, Cape Verde v Burkina Faso
Cameroon
Njie Enow (Mkuu wa Michezo, Televisheni ya Redio ya Cameroon): Miaka mitatu iliyopita Cameroon iliondoka kwenye Kombe la Mataifa katika awamu ya 16 bora, na lengo kuu la wenyeji litakuwa kunyakua kombe linalotamaniwa zaidi barani kwa mara ya sita.
Mreno Antonio Conceicao amekuwa akiongoza tangu Septemba 2019, na anapenda kudhibiti michezo kuanzia mwanzoni. Chini yake, Cameroon imerejea kwenye mchezo wa hali ya juu ambapo mabeki wa pembeni wanatarajiwa kujilinda na kushambulia kwa viwango sawa.
Ngome ya The Indomitable Lions iko kwenye safu ya kiungo cha kati, ambapo wamejaa vipaji vinavyoweza kutawala kumiliki mpira na kuongoza kasi ya mchezo. Mchezaji wa Napoli Andre-Frank Zambo Anguissa anaonekana nyota akiwa na uwezo wa kuchagua pasi katika nafasi zilizobana na nguvu anazoleta uwanjani.
Kikosi cha ushambuliaji cha Cameroon kimewekwa vyema huku Eric Maxim Choupo-Moting wa Bayern Munich akiwa mfalme, huku Karl Toko Ekambi (Lyon) akipewa majukumu zaidi.
Licha ya kurejea uwanjani tu mwezi Novemba baada ya kufungiwa kwa muda mrefu, mlinda lango wa Ajax Andre Onana bila shaka ndiye kipa chaguo la kwanza na ushujaa wake wakati wa mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia 2022 dhidi ya Ivory Coast bila umeonyesha uwezo wake.
Burkina Faso
Moussavou Billa (Sports journalist, Ouagadougou): Baada ya kukosekana mwaka 2019, Burkina Faso wanataka kusahau mashindano ya mwisho ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Misri na wamefanya bidii.
Kama wapinzani wao watatu katika Kundi A, Burkina Faso wako katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya 16, kabla ya kuvinjari msururu uliosalia ambao utawasilishwa wakati wa fainali.
Kikiwa kimeletwa kwenye michuano hiyo na wachezaji wa kizazi kipya akiwemo Herve Koffi, Edmond Tapsoba, Issa Kabore, Bertrand Traore na Gustavo Sangare, kikosi hicho kitafanya kila kitu ili kutojutia.
Mbali na ubora wao, Stallions pia watakuwa na matumaini ya kuboreshwa kwa mbinu ya kiakili - baada ya kuleta mwanasaikolojia mapema mwaka huu kusaidia timu kuzingatia kufikia malengo yake.
Ethiopia
Kaleb Moges (mwandishi wa habari wa BBC Amharic): Baada ya kukosekana kwa miaka tisa, Afcon 2021 ni fursa nzuri kwa kocha Wubetu Abate na kikosi chake kuonyesha kile ambacho Ethiopia, mmoja wa wanachama waanzilishi wa Caf, watakuwa nacho.
Abate ndiye mpangaji mkuu wa kandanda ya Ethiopia inayovutia kwa mguso mmoja. Kiungo wa kati Shemelis Bekele na nahodha Getaneh Kebede wanaongoza kikosi huku nyota chipukizi Abubeker Nasir, mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Ethiopia 2020-21, akiwa mmoja wa wale wa kutazamwa.
Wubetu alikuwa thabiti katika mtindo wake wa uchezaji katika mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia na Kombe la Mataifa kwa safu ya 4-3-3 na Nasir, pamoja na Kebede na kiungo mshambuliaji Dawa Hotessa, wanaweza kuwa hatari kwa wapinzani.
Kutinga hatua ya 16 bora itakuwa hatua kubwa kwa Ethiopia, timu ambayo bado inaendelea kujiimarisha chini ya Wubetu, lakini itawafurahisha mamilioni ya Waethiopia ndani na nje ya nchi kutazama timu yao ikicheza katika kinyang'anyiro cha ubingwa wa bara.
Cape Verde
Lucio Antunes (bosi wa zamani wa Cape Verde): Kandanda ya Cape Verde ilibadilika kutoka 2013 na kuendelea. Tulipata uzoefu wetu wa kwanza kwenye Afcon, ambao ulifanya soka yetu kujulikana kote Afrika na Ulaya pia.
Shirikisho la soka lilikuwa na mradi na tulipoanza, Cape Verde ilikuwa ya 126 katika viwango vya Fifa na tuliendelea hadi kufikia nafasi ya 27. Tunajivunia kazi ambayo shirikisho limekamilisha hadi sasa.
Natumai kuwa kila kitu kinakwenda sawa kwa timu yetu. Tuna wachezaji wazuri, ingawa wengi bado ni wachanga na hawana uzoefu katika Afcon. Kocha wetu ni mwerevu sana, mzoefu, na anailewa soka ya Afrika vyema. Kikundi kiko imara - tumejipanga katika ulinzi na na ile ya mashambulizi.
Cameroon ndiyo timu inayopendwa zaidi, na sisi na Burkina Faso tutalazimika kupigania nafasi katika raundi inayofuata. Ethiopia ndiyo timu dhaifu katika kundi lakini inastahili heshima yetu.
Ninaamini tutafika hatua ya makundi lakini kutegemeana na wapinzani katika hatua ya 16 bora tunaweza kwenda mbele kidogo. Nina imani.
0 Comments