BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATATU TAREHE 03/01/2022

 Mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 28, hana furaha kuwa Chelsea na huenda akajaribu kuungana na kocha wake wa zamani Antonio Conte katika klabu ya Tottenham msimu wa joto. (Gazzetta Dello Sport - in Italian)


Barcelona huenda wakampeana winga wa Ufaransa wa miaka 24 Ousmane Dembele kwa Manchester United katika mkataba wa utakaowawezesha kumpata mshambuliaji wa mashetani wekundu Mfaransa Anthony Martial, 26. (Ara - in Catalan)

Manchester United wana matumaini ya kumsajili kiungo wa kati wa Ungereza Declan Rice kutoka West Ham na inasemekana hatua hiyo imechochewa na kiwango cha hivi majuzi cha uchezaji wa nyota huyo, ambacho kimeifanya klabu hiyo ya London kukaribia maeneo ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa. Manchester City na Chelsea wamekuwa wakivutiwa na mchezaji huyo wa miaka 22-kwa muda mrefu. (Sun)

Declan Rice celebrates

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Maelezo ya picha,

Declan Rice akishangilia kufunga bao

Newcastle wanataka kuwasajili wachezaji karibu sita dirisha la usajili litakapofunguliwa mwezi huu wa Januari na wana matumaini ya kumpata kiungo wa safu ya kulia na nyuma wa Atletico Madrid na Uingereza Kieran Trippier, 31, na mchezaji wa pili kabla ya mechi yao dhidi Watford Januari 15. (The I)

Tottenham na West Ham ni miongoni mwa klabu zinazomtaka mshambuliaji wa Uhispania Adama Traore, 25, ambaye Wolveswako tayari muuza kwa pauni milioni 20 kufadhili bajeti yao ya uhamisho. (Telegraph - subscription required)

Meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti amependekeza klabu hiyo ya Uhispania itasubiri hadi msimu wa joto kufanya harakati za kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, 23. Mshindi huyo wa Kombe la Dunia la Ufaransa sasa yuko huru kufanya mazungumzo na timu nyingine kwani kandarasi yake inaisha mwishoni mwa msimu. (Goal)

Kylian Mbappe

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Liverpool n AC Milan wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Guinea Aguibou Camara,20, kutoka klabu ya Ugiriki ya Olympiakos. (Calciomercato - in Italian)

Aston Villa ndio klabu ya hivi punde zaidi ya Ligi ya Premia kuhusishwa na kiungo wa kati wa Borussia Monchengladbach ya Uswizi Denis Zakaria, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 pia akinyatiwa na Liverpool, Leicester City, Arsenal na Everton. (Mail)

Post a Comment

0 Comments