Brentford wanakaribia kukamilisha masharti ya mkataba wa miezi sita na kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, huku The Bees wakiwa katika harakati ya kufanya uangalizi kuhusu utayari wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kucheza. (Sky Sports)
Wakati huohuo, Vlahovic ameshutumiwa kwa kupuuza simu za klabu za mtendaji mkuu wa Fiorentina Joe Barone kufuatia taarifa ya The Gunners kutaka kumnunua mshambuliaji huyo wa Serie A. (Metro)
Mpango wa Arsenal kumnunua mshambuliaji Dusan Vlahovic, 21, umekuwa mgumu zaidi baada ya Juventus kumletea mmiliki wa Fiorentina Rocco Commisso ofa pinzani kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Serbia. (Times)
Liverpool wanamfuatilia Eduardo Camavinga katika klabu ya Real Madrid kwa kuwa wamekuwa wakivutiwa na kiungo huyo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 19 kwa muda. (El Nacional - in Spanish)
Kiungo wa kati wa Uingereza Jesse Lingard, 29, anatafuta uhamisho wa mkopo kutoka Manchester United katika dirisha la uhamisho la Januari lakini pia yuko tayari kumaliza kandarasi yake Old Trafford.(Manchester Evening News)
Tottenham wako tayari kumuuza mchezaji wa Uingereza Dele Alli na mchezaji wa kimataifa wa Argentina Giovani Lo Celso, wote wenye umri wa miaka 25, baada ya wachezaji hao wawili wa kiungo kuachwa nje ya kikosi cha Antonio Conte kwa mchezo dhidi ya Chelsea Jumapili. (Goal)
Spurs wamefanya mpango wa kutaka kumsajili winga Ollie Tanner mchezaji anayecheza katika timu ambayo haiko katika madaraja ya rasmi ya soka, Brighton nao wanamuwinda nyota huyu. (Athletic - subscription required)
Newcastle United wanakaribia kumsajili mlinzi wa kushoto wa Uholanzi Mitchel Bakker, 25, kutoka Bayer Leverkusen.(Mirror)
Arsenal wamekubali makubaliano ya mkataba wa mkopo hadi mwisho wa msimu wa kiungo wa kati wa Juventus na Brazil Arthur Melo, 25. (90min).
Liverpool inamfuatilia winga wa Fulham mwenye umri wa miaka 19 na timu ya taifa ya Uingereza Fabio Carvalho.(Fabrizio Romano)
Matumaini ya Newcastle ya kumsajili mshambuliaji wa Atalanta Duvan Zapata yameongezewa nguvu kutokana na nia ya timu hiyo ya Serie A kumtoa kwa mkopo nyota huyo wa kimataifa wa Colombia mwenye umri wa miaka 30 kwa takriban £8m. (Kioo kupitia HITC)
0 Comments