BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMATATU TAREHE 03/01/2021

 Newcastle wamewasiliana na Arsenal na kuwasilisha pendekezo la kumtaka kwa mkopo mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, mwenye umri wa miaka 32, kwa muda wote uliosalia, kwa nia ya kumnunua kwa pauni milioni 20 majira ya joto.(Sunday Mirror)



The Magpies wamenukuliwa zaidi ya £50m kwa mshambuliaji wa Benfica na Uruguay Darwin Nunez, 22.(The I)

Maafisa wa Newcastle wana amini kwamba dili la kumnunua beki wa pembeni wa Atletico Madrid na Uingereza Kieran Trippier, mwenye umri wa miaka 31, litakamilika siku chache zijazo. (Sunday Telegraph)

c
Kiungo wa kati wa Chelsea na England mwenye umri wa miaka 21 Conor Gallagher - ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Crystal Palace anawindwa kwa pauni milioni 50 na Paris St-Germain.(Sunday Telegraph)Everton wamepewa ofa ya mchezaji wa Barcelona na Brazil Philippe Coutinho, 29, huku meneja Rafael Benitez akitaka kumuongeza beki wa kulia wa Rangers na Scotland Nathan Patterson, 20, kwenye kikosi chake.(Mail on Sunday)
mHata hivyo, mzozo kati ya kiungo wa kati wa Uholanzi Donny van de Beek na wakala wake wa zamani unamaanisha kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 hana uwezekano wa kuondoka Manchester United mwezi Januari. (Sunday Mirror)Bayer Leverkusen wanataka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Muingereza Eddie Nketiah, 22, ambaye atakuwa mchezaji huru majira wa joto. (Sun on Sunday)
Leicester city wapo mbioni kumsajili beki wa Ghana Abdul Mumin, 23, kutoka Vitoria Guimaraes ya Ureno. (Mail on Sunday)
m

Mshambulizi wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 21, amewaambia mashabiki kwamba atacheza Uhispania siku zijazo. (AS - in Spanish)

Wakati huo huo, beki wa kulia wa Leeds Muingereza Cody Drameh, 20, yuko kwenye mazungumzo na Nottingham Forest kuhusu uhamisho wa mkopo. (Football Insider)

Liverpool itasajili mshambuliaji mpya katika dirisha dogo la usajili la Januari ikiwa fursa ya uwekezaji wa muda mrefu wa wachezaji itapatikana. (Anfield Watch)

Manchester United na Liverpool wote wanavutiwa na mlinzi wa Leeds United wa Uingereza aliye chini ya umri wa miaka 21 Charlie Cresswell, 19.

Watford wana mikataba ya kumnunua beki wa kushoto wa Nice na Ivory Coast Hassane Kamara, 27, na kiungo wa kati wa Eupen na DR Congo Edo Kayembe, 23, kwa £4m kila mmoja.(The Athletic - subscription required)

Mshambulizi wa Paris St-Germain na Argentina Mauro Icardi, 28, anatarajiwa kujiunga na Juventus kwa mkataba wa mkopo wa miezi sita, kukiwa na kipengele cha kumnunua.(Pedro Almeida on Twitter)

Post a Comment

0 Comments