BETI NASI UTAJIRIKE

MWAMUZI FRANK KOMBA AZIDI KUPENYEZA KIMATAIFA

Mwamuzi nambari moja nchini Tanzania upande wa Soka  ,Frank Komba ameendelea kujizolea umaarufu barani Afrika kwa uwezo mkubwa anaouonyesha kila siku anapopangiwa majukumu ya kuchezesha mechi mbalimbali.


Mwamuzi  huyo kwa sasa yupo nchini Cameroon kwenye michuano ya CAF 2021 michuano inayokutanisha mataifa 32 ya Africa na amefanikiwa kuchezesha michezo miwili kama Refa namba mbili kwenye michezo ya Comoro na Gabon mchezo uliomalizika kwa Gabon kushinda bao 1-0 na ule wa Gabon na Morocco uliomalizika kwa mabao 2-2.

Kutokana na umakini na umahiri wa Frank ,CAF wamemuongezea majukumu mengine na sasa atakuwa miongoni mwa Waamuzi watakaochezesha mchezo wa hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Africa kati ya Raja Casablanka ya Morocco na Amazulu ya Afrika Kusini mchezo utakaopigwa dimba la Mohammed VCasablanca Morocco February 12 ,2022 

Post a Comment

0 Comments