BETI NASI UTAJIRIKE

MSEMAJI WA SIMBA AANZA KWA KUWATUPIA VIJEMBE YANGA

 Hatimaye Afisa habari wa klabu ya Simba Ahmed Ally ameanza rasmi kazi yake ndani ya klabu hiyo mara baada tu baada ya uteuzi.Ahmed Ally aliyeteuliwa majira ya saa 4 asubuhina uongozi wa klabu ya Simba ameianza safari kuelekea Zanzibar kuifuata timu hiyo iliyoondoka majira ya saa 3 asubuhi kuelekea Zanzibar na kuwasili saa 6 mchana  kwenye michuano ya Mapinduzi Cup iliyokwisha anza . 

Mbali na ratiba hiyo amewaonya wapinzani wao kwenye michuano hiyo kwamba wanakwenda kubeba kombe hilo ili kuonyesha ukubwa wa klabu hiyo na kuongeza kuwa baadhi ya klabu zinategemea kubeba kombe hilo pekee msimu huu. 

Ahmed Ally ametafsiriwa kwamba kauli hiyo ni dongo kwa Yanga kwani wao ni mabingwa watetezi wa kombe hilo na sasa wanahangaika kurejesha kombe la ligi kuu waliloshindwa kunyakua kwa msimu wa nne mfululizo.

Akiwa ndani ya Boti ya Azam Marine Ahmed Ally ametoa ratiba yake kwa siku ya leo kuanzia lengo la safari Zanzibar na mambo atakayo yafanya akiwa huko. ameandika 

Safari kuelekea Zanzibar 🦁🦁Safar kwenda kuchukua Kombe la Mapinduzi.Yess ni rahisi na inawezekana tupo tayari.Tunafahamu wengine hili ndo Kombe lao pekee la kujivunia hivyo tunalichukua Ili tuwakumbushe kuwa sisi ni Wakubwa kwao.Saa 8:20 Insha Allah, Nitakua Forodhani na baadae saa 11:15 nitahudhuria mazoezi ya kwanza ya timu katika Uwanja wa Mao tse Tung🦁🦁

Post a Comment

0 Comments