Mshabuliaji wa PSG Kylian Mbappe ameuanza mwaka 2022 kwa staili ya kipekee baada ya kufunga mabao matatu dhidi ya Vannes kwenye mchezo wa kombe la Ufaransa Coupe de France
Beki Kimpembe alikuwa wa kwanza kufungua nyavu kwenye mchezo huo dakika ya 28 hukuKylian Mbappe akifunga bao la pili dakika ya 59,71 na 76 na kuwafanya PSG kushinda mabao 4-0. Hat trick ya Mbappe ni ya kwanza kwa mwaka huu 2022 akiwa ndiye mchezaji wa kwanza ulaya kufunga hat trick mwaka huu lakini pia alitumia dakika 18 tu kuweka rekodi hiyo
Mchezaji Lionel Messi ataendelea kuwa nje ya uwanja baada ya kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona yeye pamoja na wachezaji wenzake watatu wa timu hiyo.
0 Comments