advertise with us

ADVERTISE HERE

MATOKEO YA YA MECHI ZA MAPINDUZI CUP HAYA HAPA

 KMKM imeanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa Taifa Jang'ombe mabao 2-1 katika mchezo wa Kundi B usiku wa Jumatatu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.


Mabao ya KMKM yamefungwa na Eliasa Suleiman dakika ya 34 na la penalti la Abrahman Othman dakika ya 45 na ushei, wakati la Taifa limefungwa na Yasir Masoud dakika ya 40.
Mechi iliyotangulia ya Kundi C baina ya Selem View na Mlandege ilimalizika kwa sare ya bila mabao.

Michuano hiyo itaendelea leo Jumanne kwa mechi mbili pia, Namungo na Yosso Boys Saa 10:05 jioni na Azam FC dhidi ya Meli 4 City Saa 2:15 usiku zote za Kundi A hapo hapo Uwanja wa Amaan.

Post a Comment

0 Comments