Kombe la Mapinduzi linaendelea siku ya leo huku kukiwa na michezo miwili ya michuano hiyo mchezo wa kwanza utakuwa ni kati ya simba na Slem View na wapili ni Yanga vs Jang'ombe
Yanga watacheza mchezo wao na Taifa Jang'ombe majira ya saa 02;15 Usiku. Mchezo huu unategemewa kuwa kivutio zaidi kwenye michuano hiyo na kuna uwezekano mshambuliaji mpya kutoka Mbeya Kwanza Crispin Ngushi akawemo kwenye kikosi hicho.Kocha Nabi hatakuwemo kwenye msafara huo na majukumu amekabidhiwa Cedric Kaze huku pia wachezaji watano wa kikosi cha kwanza watakosekana kwa sababu mbalimbali ikiwemo za kifamilia na za kimajukumu kwa timu zao za taifa
Simba watakuwa wa kwanza kukipiga na Slem View ya Zanzibar kwenye mchezo utakaopigwa dimba la Amaan Zanzibar majira ya saa 10.15 jioni na itaongozwa na kocha wake mkuu Pablo akishirikiana na Matola.Simbaitawakosa nyota wake wanne kwenye michuano hiyo akiwemo Joash Onyango,Aishi Manula na Peter Banda . Mchezo huu unakuwa wa kwanza kwa Simba kwenye michano hiyo na unategemewa kuwa kivutio kwan Simba itatumia wachezaji wengi wapya iliyowasajili dirisha hili dogo
0 Comments